Wednesday, September 24, 2014

TAMASHA LA MICHEZO SEPTEMBA 2014 SEKOMU



Ile siku iliyosubiriwa na vijana wengi karibu wa Mkoa mzima wa Tanga imekamilika kwa matayarisho yote muhimu.
Hili ni Tamasha la pekee la Kimichezo linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) kuanzia tar 23-27 Septemba 2014. Vijana wapatao 160 kutoka kanda kuu tano za Mkoa wa Tanga zinashiriki ambazo ni Kanda ya Mlalo, Kanda ya Mtae, Kanda ya Lushoto, Kanda ya Bumbuli na Kanda ya Tanga.   
Tamasha litahusisha michezo ya Riadha,Mpira wa Pete,Michezo ya kuigiza,mpira wa miguu,Mashindano ya Baiskeli na kuvuta kamba.
 Ujumbe mkuu wa YMCA-YWCA LUSHOTO

 Viwanja kwaajili ya Riadha vikotayari


Ukumbi na Jukwaa litakalotumika kwa Sanaa za maigizo lipo tayari

No comments:

Post a Comment