Thursday, October 31, 2013

MASHINDANO YA BAISKELI YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA LUSHOTO

Mashindano ya kwanza ya kihistoria yafanyika Lushoto na kufurahisha wengi waliopata nafasi kuona mashindano hayo mjini Lushoto tar 26.10.2013 kuanzia saa 2.30 asubuhi.yajulikanayo kwa jina TOUR de LUSHOTO. mashindano haya yalifanyika kwa km 13 kutoka viwanja vya sabasaba mjini hapa kupitia Ghana, Kwesimu,Kwembago,maguzoni ,IJA na kumalizikia pia viwanja vya sabasaba. Akifungua mashindano hayo mkuu wa wilaya ya Lushoto Mh. ALHAJ MAJID MWANGA aliwaasa vijana kupambana na umaskini kwa kufanya kazi katika vikundi ambavyo kwa hivyo serikali katika Wilaya yake ipo tayari kuwasaidia katika miradi ya Kilimo cha alizeti, Mbogamboga na Matunda. Aidha shughuli ufundi katika fani ya ujenzi na useremala ameahidi kuwasaidia wakiwa katika vikundi. Shime vija wa Lushoto Tengenezeni vikundi vya kazi,sio vya vijiweni.


Tupo tayari.......!!!
 Mratibu wa YMCA-YWCA LUSHOTO Rev G.Walalaze akimkaribisha Mkuu wa Wilaya 
na wageni mabalimbali.

Mkuu wa Wilaya  Mh. ALHAJ MAJID MWANGA akizungumza na Washiriki.


Kauli mbiu yetu........
 Mkuu wa Wilaya akifungua mashindano hayo kwa kuendesha Baiskeli
"............... Nimo na hamiwezi namie ni kijana" !!!!!!





 Kwenye mstari kaa tayari....................Go....

 Ngoma inagwa....................!!!!!!!!
 Kijana John Kaoneka maeneo ya Bara Lushoto
wakimbiaji Wengi wakipita kona ya maji Bara kwa mbwembwe!!!

Saturday, October 19, 2013

TOUR de LUSHOTO


MASHINDANO YA BAISKELI LUSHOTO
26TH OCTOBER 2013

Mnakaribishwa wote katika mashindano ya baiskeli yanayojulikana kama
TOUR de LUSHOTO
Yatakayofanyika tar 26 October 2013 kuanzia viwanja vya michezo Lushoto Sabasaba- Ghana-Kwesimu-Kwembago-Maguzoni-IJA Ghana –Sabasaba. Umbali wa KM13 (Kumi na Tatu).
Muda wa kuanza ni saa 1.00 asubuhi
Wote wanaohitaji kushiriki wajiandikishe katika ofisi yetu ya YMCA-YWCA Lushoto au simu 0715919103
Kila mshiriki atapewa Baiskeli ya kufanyia mashindano maadam awe na kitambulisho kinachokubalika Kiserikali (kama Leseni ya udereva au Kitambulisho cha upigaji kura au kadi ya benki au mdhamana anayekubalika.

ZAWADI NONO ITATOLEWA KWA MSHINDI WA KWANZA, PILI NA TATU.
KARIBU SANA.

Thursday, October 17, 2013

SHANGWE NA NDEREMO BAADA YA KUPOKEA VIKOMBE



Hii sura ya mwisho vijana wakipongezana kwa shamra shamra wakati wa kufunga Tamasha la michezo pamoja na Sala ya shukrani kwa Mungu kumaliza salama.


  Asante Mungu wetu katika Jina la Yesu Kristo....

 
 Sala ya shukrani baada ya mashindano kumalizika salama.
 Ni letu Ni letu.Kombe........................!!!


 
 Sisi ndio sisi Lushoto(watoto wa Mjini)

 
 Tumelipata kombe wadada wa Mlalo na Ngwelo.Haya bwana..................

MAMBO YA MISOSI NA MADIKODIKO!!!


 Ajali!!!!!

 
 KITAMU NA SODA !! Mmmmmm!!!!!!!!!!

TUSUBIRI TATAFIKA!!!

STOP POVERTY-TOKOMEZA UMASKINI



Vinywani mwa  vijana wengi  maneno haya  STOP POVERTY/TOKOMEZA UMASKINI” yalisemwa sana.Kama alivyoweka kifua chake mbele mshiriki akisomeka STOP PORVETY

 Ni kauli mbiu ya Tamasha la vijana Wilayani Lushoto lenye misingi ya kuwasaidia vijana kujitambua katika kupambana na Umaskini miongoni mwao.

Ni kweli umaskini upo miongoni mwetu je Tunajitambua?????

Shiriki kikqamilifu katika shughuli za YMCA-YWCA Lushoto utatambua mengi kuhusu maisha ya vijana na changamoto zake.

Mrabitu na mjumbe wa Bodi mr Mtangi katika Pozz na wadada katika kumsaka mshindi wa tatu wa Netball
 

 Yes. !!!!!  Lazima kieleweke mshindi wa tatu.

 

 

 Sala kwanza kabla ya Mpambano.!!!




 Ama zao Ama zetu.

  Baada ya yote Nasaha za mwisho!!!!