Monday, October 7, 2013

TAMASHA LA MICHEZO 2013 LUSHOTO



TAMASHA LA MICHEZO YA VIJANA LA FANA LUSHOTO
Na Thomas Mgonda (Lushoto)
 

Tamasha la Vijana lenye kauli mbiu TOKOMEZA UMASKINI. (STOP POVERTY)
lafanyika kwa  mafanikio makubwa  katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa. (SEKOMU) .Timu kutoka kanda nne za Wilaya ya Lushoto zilichauana vikali katika michezo mbalimbali.
Ambazo ni Kanda ya Bumbuli, Kanda ya Mtae, Kanda ya Mlalo na Kanda wenyeji Lushoto. Akifungua Tamasha hilo Mchungaji Godfrey Walalaze ambaye ni Mratibu wa  YMCA-YWCA Lushoto, aliwataka Vijana kutumia michezo katika kupambana na Umaskini kwa  kufanya kazi kwa bidii. na kuitumika jamii yao. ".....Vijana kumbukeni kuwa michezo ni ajira....." Mch. Walalaze Aliwataka Vijana Wilayani Lushoto kutobweteka katika shughuli zao za siku kwa siku ikiwepo kutimiza wajibu wao kwa familia, jamii yao na   Taifa kwa ujumla.
Aidha aliwataka vijana kucheza kwa nidhamu ,furaha na kuheshimiana kwa kila namna.
 katika michezo kwa ujumla,  timu ya kanda ya Mlalo  ya mpira wa pete iliibuka mshindi  wa kwanza na timu ya Kanda ya Lushoto iliibuka mshindi wa kwanza katika mchezo wa mpira wa miguu.

Hapa jinsi vijana walivyafalia.....

Timu za mprira wa pete toka Bumbuli na Mlalo wakikaguliwa

 Kiongozi wa YMCA madam Crala na Mr kamote katika picha ya pamoja na wachezaji
 Sala kwanza

FOOTBALL/MPIRA WA MIGUU HAOO!!!

Mratibu wa YMCA-YWCA Mch.G. Walalaze  akiwatia moyo vijana!



Tuna pendeza sana ......
 Waamuzi katika pozzz lao!!

 Mungu Tusaidie sana Mechi hii!!


No comments:

Post a Comment