Mashindano ya kwanza ya kihistoria yafanyika Lushoto na kufurahisha wengi waliopata nafasi kuona mashindano hayo mjini Lushoto tar 26.10.2013 kuanzia saa 2.30 asubuhi.yajulikanayo kwa jina TOUR de LUSHOTO. mashindano haya yalifanyika kwa km 13 kutoka viwanja vya sabasaba mjini hapa kupitia Ghana, Kwesimu,Kwembago,maguzoni ,IJA na kumalizikia pia viwanja vya sabasaba. Akifungua mashindano hayo mkuu wa wilaya ya Lushoto Mh. ALHAJ MAJID MWANGA aliwaasa vijana kupambana na umaskini kwa kufanya kazi katika vikundi ambavyo kwa hivyo serikali katika Wilaya yake ipo tayari kuwasaidia katika miradi ya Kilimo cha alizeti, Mbogamboga na Matunda. Aidha shughuli ufundi katika fani ya ujenzi na useremala ameahidi kuwasaidia wakiwa katika vikundi. Shime vija wa Lushoto Tengenezeni vikundi vya kazi,sio vya vijiweni.
Tupo tayari.......!!!
|
Mratibu wa YMCA-YWCA LUSHOTO Rev G.Walalaze akimkaribisha Mkuu wa Wilaya
na wageni mabalimbali.
Mkuu wa Wilaya Mh. ALHAJ MAJID MWANGA akizungumza na Washiriki.
Kauli mbiu yetu........
Mkuu wa Wilaya akifungua mashindano hayo kwa kuendesha Baiskeli
"............... Nimo na hamiwezi namie ni kijana" !!!!!!
Kwenye mstari kaa tayari....................Go....
Ngoma inagwa....................!!!!!!!!
Kijana John Kaoneka maeneo ya Bara Lushoto
wakimbiaji Wengi wakipita kona ya maji Bara kwa mbwembwe!!!
No comments:
Post a Comment